Ruto: Kazi ya vijana siyo tu kupiga kura

Martin Mwanje
1 Min Read

Rais William Ruto amewataka kujihadhari na wanasiasa wanaokusudia kuwatumia vibaya ili kutimiza malengo yao.  Ruto amesema vijana badala yake wanapaswa kuwazia namna ya kuanzisha miradi ambayo itawaletea kipato na kubadilisha hali yao ya maisha. “Young people are not voting machines. Kazi ya vijana si kupiga tu kura,” alisema Rais Ruto wakati wa uzinduzi wa mradi wa Nyota unaolenga kuwawezesha vijana kibiashara. Ruto akisema mradi huo ni miongoni mwa mingine iliyoanzishwa na utawala wake kutatua changamoto zinazowakumba vijana nchini. Miradi mingine ni mpango wa nyumba za gharama nafuu huku baadhi ya vijana wakienda kufanya kazi ughaibuni. Mradi wa Nyota unaohusisha vijana wapatao 820,000 unazinduliwa katika maeneo mbalimbali ya nchi huku kila kijana akipata shilingi 25,000 za kuanzisha biashara ndogo ndogo katika awamu ya kwanza. Shilingi zingine 25,000 zitakabidhiwa vijana wajasiriamali katika awamu ya pili. Hadi kufikia sasa, kiongozi wa nchi amewahutubia vijana 48,ooo kuhusu manufaa ya mradi huo ambao anasema si mkopo.

Website |  + posts
Share This Article