Rais Ruto: Jamii ya Dawoodi Bohra imechochea ukuaji wa uchumi

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Ruto atembelea jamii ya Dawoodi Bohra kwenye taasisi ya Aljamea-tus-Saifiyah.

Rais William Ruto leo Ijumaa alizuru taasisi ya Aljamea-tus-Saifiyah jijini Nairobi inayomilikiwa na jamii ya Dawoodi Bohra.

Kiongozi wa taifa aliipongeza jamii hiyo ya Dawoodi Bohra kwa mchango wake katika maendeleo ya taifa hili hususan katika sekta za makazi, huduma za afya, na elimu.

Aidha Rais Ruto alisisitiza kujitolea kwa serikali kuimarisha sekta ya elimu kama nguzo kuu ya  mabadiliko, akilenga kuhakikisha asilimia 60 ya wanafunzi wanapata ujuzi katika sayansi, teknolojia, uhandisi, na hisabati. 

Alisema hatua hii itafanikisha upatikanaji wa guvu kazi inayoweza kuimarisha uchumi wa taifa hili.

Rais Ruto aliongeza kuwa maono hayo yanaungwa mkono na miradi mikubwa ya miundombinu, ikiwa ni pamoja na kuzalisha megawati elfu kumi za nishati, kujenga kilomita elfu 30 za barabara, kujenga uwanja wa ndege wa kisasa, na kuboresha sekta ya afya.

Website |  + posts
Share This Article