Watu kadhaa wamehofiwa kufariki baada ya ndege ndogo kuripotiwa kuanguka na kuwaka moto katika eneo la Kowachocha huko Malindi, kaunti ya Kilifi.
Yamkini watu wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na ajali hiyo.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana.
Polisi wamefika eneo hilo wakati shughuli za uokozi zikiendelea.
Hata hivyo, mamlaka husika hazijathibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Tutakuletea taarifa za kina punde tukizipokea