Namwamba ateuliwa Balozi wa Uganda, Maangi ahamia Ubelgiji

Dismas Otuke
0 Min Read

Waziri wa zamani wa Michezi Ababu Namwamba ameteuliwa kuwa Balozi mpya wa Kenya nchini Uganda. Joash Maangi aliyekuwa akihudumu katika nafasi hiyo ameteuliwa kuwa Balozi wa Kenya nchini Ubelgiji.

Hadi uteuzi wake, Ababu amekuwa Balozi wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP), huku Maangi akihudumu kama Balozi wa Kenya nchini Uganda.

Maangi anaelekea jijini Brussels kurithi wadhifa ulioshikiliwa na Dkt. Bitange Ndemo.

Website |  + posts
Share This Article