Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda anaongoza kura za Urais kutokana na matokeo ya asilimia 45 ya vituo vya kupigia kura.
Museveni wa chama cha National Resistance Movement (NRM) amepata asilimia 76.25, ya kura zilizohesabiwa kutoka vituo 22,758.
Robert Kyagulanyi wa chama cha National Unity Platform (NUP) ni wa pili akiwa na kura 1,312,047, sawia asilimia 19.85 ya kura zilizohesabiwa.
Uganda ina wapiga kura 21,649,067, na jumla ya vituo vya kupigia kura 50,739, vilivyosajiliwa kulingana na takwimu za mapema mwaka huu.
Rais Museveni mwenye umri wa miaka 80 na aliyetwaa uongozi mwaka 1986, anatarajiwa kutangazwa mshindi kwa muhula mwingine.