Mulamwah ajitetea baada ya uvumi kusambaa kwamba alinunua gari kwa mkopo

Jamaa mmoja alikuwa amedai kwenye mtandao wa TikTok kwamba msanii huyo amekuwa fukara na ameshindwa kulipa mikopo mbali mbali anayodaiwa.

Marion Bosire
2 Min Read

Mchekeshaji David Oyando maarufu kama Mulamwah amejitetea baada ya uvumi kusambazwa mitandaoni kwamba alinunua gari kwa mkopo na limetwaliwa kwa kushindwa kulipa.

Mulamwah alichapisha stakabadhi ya umiliki wa gari hilo kudhibitisha ni lake, huku akiorodhesha vyanzo kadhaa vya mapato.

Alitaja akaunti ya YouTube, pikipiki za uchukuzi wa abiria almaarufu bodaboda ambazo ni 40, midundo ya simu almaarufu Skiza Tunes pamoja na ushirikiano wa kutangazia kampuni mbali mbali bidhaa.

Oyando alitaja pia kazi yake ya redio katika kituo cha Milele Fm pamoja na kilimo.

Msanii huyo alichpaisha picha za nyumba yake ambayo inaendelea kujengwa huko Kitale na za gari hilo aina ya Mercedes Benz akisema kwamba kwa sababu mambo ni magumu, haimaanishi hayawezekani.

“Tujifunze kuthamini juhudi za kila mmoja na kusherehekea mafanikio yao. Wakati wote jivunie hatua ndogo unazopiga maishani.” aliandika Mulamwah kwenye Facebook.

Alifafanua kwamba huwa hachapishi mafanikio yake kama njia ya kujionyesha kwani hakuna mashindano bali huwa anachapisha kuonyesha kwamba hali inaweza kubadilika.

Alihimiza wafuasi wake akisema mtu anaweza kuanzia chini na akapata mafanikio bora anatia bidii na wachukulie machapisho kama himizo na wala sio kejeli.

Mulamwah alimalizia kuwatupia maneno wale ambao wanataka kudhibitisha iwapo stakabadhi aliyochapisha ya kumiliki gari ni halali.

Jamaa mmoja alikuwa amedai kwenye mtandao wa TikTok kwamba msanii huyo amekuwa fukara na ameshindwa kulipa mikopo mbali mbali anayodaiwa.

Share This Article
Leave a Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *