Morocco yafuzu fainali ya AFCON baada ya subira ya miaka 21

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wa makala ya 35 ya kindumbwendumbwe cha kuwania Kombe la mataifa ya Afrika Moroccoc walifuzu kwa fainali baada ya kuwalemea Nigeria mabao 4-2, kupitia penati kufutia sare tasa ndani ya dakika 120.

Nusu fainali hiyo ilipigwa Jumatano usiku katika uchanjaa wa Prince Moulay Abdellah mjini Rabat.

Morocco almaarufu Simba wa milima ya Atlas, wanaowinda kombe la pili tangu mwaka 1976, watamenyana na Simba wa Teranga kutoka Senegal katika fainali ya Jumapili .

Aidha ilikuwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004, kwa Morocco kufuzu kwa fainali ya kombe hilo.

Senegal walijikatia tiketi kwa fainali baada ya kuwazidia maarifa Misri bao moja kwa bila katika nusu fainali ya kwanza iliyosakatwa katika kiwara cha Tanger.

Website |  + posts
Share This Article