Marjan Hussein Marjan aondoka IEBC

Tom Mathinji
1 Min Read
Marjan hussein Marjan aondoka IEBC.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC), Marjan Hussein Marjan, amejiuzulu.

Kujiuzulu kwa Marjan, kunafuatia mpito ulioafikiwa na pande zote kutoka kwenye wadhifa wake wa katibu wa tume hiyo aliye pia Afisa Mkuu Mtendaji.

Kupitia kwa taarifa iliyotiwa saini na mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon, ilisema tume hiyo sasa itamteua kaimu Afisa Mkuu Mtendaji kuhakikisha shughuli za tume hiyo zinaendelea kama kawaida.

“Hatua hiyo ni kuambatana na kujitolea kwa IEBC kuhakikisha mpito shwari katika kutekeleza majukumu ya kikatiba ya tume hiyo ikiwa ni pamoja na kuandaa chaguzi na kubainisha mipaka miongoni mwa majukumu mengine muhimu,” ilisema taarifa hiyo.

Aidha tume hiyo ilimpongeza Marjan kwa uongozi wake shupavu tangu alipoteuliwa Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume hiyo mwaka 2022.

Website |  + posts
Share This Article