Mama Ida Odinga ateuliwa Balozi wa Kenya katika UNEP

Tom Mathinji
1 Min Read
Mama Ida Odinga.

Rais William Ruto, amemteua Dkt. Ida Odinga, mjane wa aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga, kuwa balozi na mwakilishi wa kudumu katika Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa  (UNEP).

Iwapo uteuzi wake utaidhinishwa na Bunge la Taifa, Ida atachukua nafasi iliyoshikiliwa awali na Ababu Namwamba, ambaye ameteuliwa balozi wa Kenya nchini Uganda.

Huku akitangaza uteuzi huo Ijumaa jioni, Mkuu wa Utumishi wa Umma Felix koskei, alimtaja Ida kuwa msoni, kiongozi, na mtetezi wa haki ya kijamii na usawa wa kijinsia.

“Huduma yake katika utumishi wa umma, uliodhihirishwa na ujasiri wake, kujitolea na jinsi alivyokabiliana na changamoto, umesababisha achaguliwe kama mwakilishi wa kudumu katika Mpango wa Mazingira wa Umoja wa Mataifa,” alisema Koskei kwenye taarifa hiyo ya uteuzi.

Iwapo Bunge la Taifa litaidinisha uteuzi wake, Ida anatarajiwa kupaza sauti ya Kenya kuhusu maswala ya mazingira na kuimarisha uongozi wa kidiplomasia wa Kenya katika maswala ya mazingira, na jukumu lake muhimu kama mwenyeji wa afisi za UNEP.

Rais William Ruto amewasilisha jina la Ida Odinga katika Bunge la Taifa ili asailiwe na kuidhinishwa kwenye wadhifa huo.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article