Majambazi waiba mbuzi 1,200 na ng’ombe 200 Laikipia

Tom Mathinji
1 Min Read
Majambazi waiba mbuzi 1,200 na ng'ombe 200 Laikipia.

Hali ya wasiwasi imetanda katika msitu wa Doldol, Laikipia Kaskazini kaunti ya Laikipia, baada ya wezi kuwaiba mbuzi 1,200 na ng’ombe 200.

Kulingana na wakazi, majambazi hao wanaaminika wamejificha katika mlima Losos kaunti ya Isiolo, na kwamba huenda wanapanga mashambulizi zaidi.

Uvamizi huo ulilenga maeneo ya Salamba, Seek na Naibung’a na kusababisha wanafunzi kuondoka shuleni kuwafuata wazazi wao ambao wanawahamisha mifugo wao.

Wengi wa wachungaji mifugo wanadaiwa kuhama Doldol kuelekea Nanyuki.

Msimamizi wa hifadhi ya Upper Naibung’a, Peter Kilua, amesema msitu wa Mukogodo umetangazwa kuwa eneo lenye misukosuko na licha ya hakikisho la serikali kuwa oparesheni ya kijeshi ya kuwafurusha majambazi kutoka humo itatekelezwa, hakuna lolote lililofanyika kufikia sasa.

Hali katika eneo hilo inasalia kuwa tete huku viongozi wakiendelea kutoa wito wa kuongezwa kwa maafisa wa usalama ili kurejesha utulivu.

Website |  + posts
TAGGED:
Share This Article