Tume ya Maadili na vita dhidi ya Ufisadi (EACC), imewakamata maafisa watatu wa polisi wa trafiki kwa madai ya kupokea hongo kwenye kizuizi cha barabarani katika eneo la Kyumbi kaunti ya Machakos.
Maafisa hao David Gitonga, Herman Echakara na Lucy Ekwan, wanaotoka katika kituo cha polisi cha Kyumbi kaunti ya Machakos, walifikishwa katika afisi za EACC mjini Machakos kuandikisha taarifa.
“Operesheni hiyo ni sehemu ya juhudi za tume hii za kukabiliana na ufisadi na kuimarisha maadili, uwajibikaji na utaalam katika utumishi wa umma,” Ilisema EACC kupitia kwa taarifa.
Maafisa kadhaa wamekamatwa kwenye operesheni za EACC, kufuatia kuripotiwa kwa visa kadhaa za ufisadi hususan kutoka kwa wananchi.
“EACC inawahimiza wananchi kuripoti visa vyovyote vya ufisadi kwa tume hiyo kama sehemu ya jukumu la pamoja la kuimarisha maadili na kuboresha imani ya umma,” iliongeza EACC.
