Chifu na mwalimu wauawa huko Garissa

KNA
By
KNA
1 Min Read

Watu wawili,chifu na mwalimu, waliuawa leo alfajiri baada ya watu wanaoaminika kuwa Al Shabaab kutekeleza shambulizi baya katika mji wa Hulugho, kaunti ya Garissa.

Chifu huyo wa Hulugho kwa jina Hulugho Abdi Fatah Gani alipigwa risasi na waasi hao waliovamia makazi yake saa kumi alfajiri.

Wavamizi hao ambao idadi yao haijabainika, wanaripotiwa kumpiga risasi chifu huyo kwa karibu mbele ya familia yake na baadaye wakachoma gari lake kabla ya kuondoka.

Walipokuwa wakiondoka, walimpiga risasi mwalimu ambaye alitambuliwa kama Stephen Musili, mkazi wa eneo lililoshambuliwa.

Kulingana na wenyeji, Chifu Abdi amekuwa akilengwa na waasi hao kwa muda kutokana na juhudi ambazo amekuwa akiendeleza za kumaliza wanachama wa Al Shabaab na washirika wao kutoka eneo hilo.

Kamishna wa kaunti ya Garissa Mohamed Mwabudzo amethibitisha tukio hilo.

KNA
+ posts
Share This Article