Halmshauri inayodhibiti michezo ya kamari humu nchini (BCLB), ikishirikiana na chama cha wamiliki wa kampuni za kamari nchini (Agok), wamezindua kampeini ya kitaifa ya kuhamasisha umma kuhusu maadili ya kucheza kamari.
Uhamasisho huo umezinduliwa leo katika chuo cha mafunzo ya wafanyakazi wa reti (RTI) mtaani South B.
Kulingana na mwenyekiti wa BCLB, Jane Mwikali, kampeini hiyo ijulikanayo kama Chukua Control, itaendeshwa kwa kipindi cha miezi sita ijayo .
Hatua hii ni ya hivi punde baada ya BCLB, kupiga marufuku matangazo yote ya kueneza kamari kupitia kwa vyombo vya habari.
Lengo kuu la kampeini hiyo ni kuhumiza umuhimu wa kushiriki kamari.